Mashairi
Aso chake (Mahmoud Mau)
User Rating: / 19
PoorBest 
Mashairi

ASO CHAKE

(1) Aso chake hana lake,
wala hatambulikani
Na hata kwa mola wake,
aso chake hunenani?

(2) Aso chke ni muinga,
angawa mno mwerevu
angawa fundi kupanga,
hambiwa ni mpumbavu
kwenye mambo humtenga,
angaliya nazi mbovu !

(3) Aso chake si mzuri,
angawa kama mwezi
Aso chake si hodari,
angawa mno muyuzi
Aso chake ni jauri,
angawa ni mtukuzi!

(4) Aso chake ni fidhuli,
na sawa yake ni jongo
Anga nena yalo kweli,
huwambiwa ni mrongo
Angawa huona mbali,
huonekana nitongo!

(5) Aso chake ni mchafu,
naangawa maridadi
Na aso chake ni dufu,
angawa shekhe
Biladi Hapati umaarufu,
angawa mwenyeji jadi.

(6) Aso chake rai hana,
angawa ni SAQARATI
Aso chake akinena,
wakusikiza hapati
Walo wake humkana,
hata muda wa mauti

(7) Mwenye chake ndiye Bwana,
mwerevu mwenye busara
Angawa hana maana,
hupowa yeye bendera
Husoza nasi huwoba!
Hini ni kuu hasara.

(8) Na hini ndiyo sababu,
ya mambo kuharibika Zimetuzidi taabu,
Nakwetu kumefujjika
Na tama ya karibu,
hapana ketengezeka

(9) Ni sharuti tubadili,
nafikira tugeuze Wakisimama wawili,
mwenyechake sishunduze
Tumpe mwenye akili,
ili chombo achoweze.

 

 

 


Mashairi

MOLA NDIYE WAKUTUKIDHI (Alamin Somo)

News image

MOLA NDIYE WAKUTUKIDHI. 1. Risala 'naye pendeza,kwa kazi yako njema. Hebu na leo tokeza,nami...

Readmore

HAYAWI ILLA YATENDWE(Ahmed M.Msallam)

News image

(1) NATAKA MNO BAJUNI WAWE WEMA WALIMWENGUWAWE HWINGIA MATONI MWA AJINABI NA MWANGUWAJAE TELE...

Readmore

NALILIA UBAJUNI (Mbwana Masuo)

News image

NALILIA UBAJUNI Nalilia ubajuni, ilahi achusitiri kivakumbuka moyoni,   dua dhangu hukithiri Mungu atachuawini,  achupe kula la...

Readmore

More in: Alamin Somo, Ahmed Muhammad Msallam, Mbwana Masuo

100%
-
+
12
Show options